(ABNA24.com) Sayyid Abbas Mousavi alisema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari wa ndani na wa nje hapa mjini Terah na kueleza kwamba, ana matumaini kuwa, kama ilivyo Iran, walimwengu nao watafuatilia suala la kuweko dunia isiyo na vitendo vya utumiaji mabavu.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria "Siku ya Dunia Isiyo na Utumiaji mabavu Wala Misimamo ya Kufurutu Asda" ambayo inaadhinmishwa kesho tarehe 18 Disemba kote duniani na kusema kuwa, utawala wa Saudi Arabia unapaswa kuachana na miamala yake ya kindumakuwili na kupokea mkono wa urafiki ulionyooshwa na Iran na mataifa mengine ya eneo.
Sayyid Abbas Mousavi ameashiria mpango uliopendekezwa naJamhuri ya Kiislamu ya Iran wa "Ubunifu wa Amani ya Hormuz" na kkuusisitiza kwamba, watawala wa Saudi Arabia wanapaswa kufahanmu kuwa, hatua yao ya kuwaita wageni na kurundika silaha haisadii chochote katika kuleta amani na usalama wa eneo.
Amezungumzia pia kadhia ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusema kwamba, madola ya Ulaya yaliyobakia katika makubalianop hayo yanapaswa kutumia vyema fursa iliyobakia na kutekeleza ahadi zao katika uwanja huo.
..........
340